Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / HARMONIZE NDANI YA KAMATI MPYA YA NDANDA FC

HARMONIZE NDANI YA KAMATI MPYA YA NDANDA FC

| No comment
Image result for HARMONIZE

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gilasius Byakanwa ameamua kuuweka pembeni uongozi wa Ndanda SC uliopo sasa akidai kuwa uongozi huo umeshindwa kuiendesha timu hiyo kiasi cha kuishia kuwa “ombaomba” kila msimu.


Byakanwa ambaye amechukua hatua hiyo akiwa kama mlezi wa timu, ameamua kuunda kamati maalum ya watu 10 itakayosimamia timu hiyo kwa kipindi cha msimu wa ligi kilichosalia.

Image result for HARMONIZEMkuu huyo wa mkoa pia amesema atamuomba msanii Harmonize kuwa sehemu ya kamati hiyo endapo ataridhia.

Wanaounda kamati hiyo ni Laurant Paul Werema ambaye atakuwa Mwenyekiti, Stanley Milanzi, Athuman Kambi, Raymond Kasuga, Joseph Peneza, Badwin Masawe, Mohamed Remtulah, Mohamed Nassor, Potensi Rwiza na Said Ally.

“Kuendesha timu kunahitaji pesa, kwahiyo huwezi kuwa na viongozi ambao wakikutana hawawezi hata kununua maji kwaajili ya wachezaji,” amesema Byakanwa.