Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / DIAMOND PLATNUMZ ASIMAMISHA SHUGHULI ZOTE TANDALE

DIAMOND PLATNUMZ ASIMAMISHA SHUGHULI ZOTE TANDALE

| No comment

Mwanamuziki Naseeb Abdul, 'Diamond' amesimamisha shughuli zote za Tandale na kuwafanya mamia ya wakazi wa kitongoji hicho kujitokeza kwa wingi kwenye Uwanja wa Magunia kusheherekea siku yake ya kuzaliwa.



Mamia ya wanawake wamefurika kwa ajili ya kuandikisha majina ya kupatiwa mitaji na bima za afya za watoto.


Uandikishaji huo umeanza tangu asubuhi katika uwanja huo, ambao wanawake wameonekana kuwa katika foleni kwa watu watatu tofauti waliopewa kazi ya kuandika majina.


Shughuli nyingine atakazofanya Diamond ni pamoja na kugawa bodaboda kwa vijana, kukarabati shule zote za msingi za Tandale akianza na ile aliyosoma, kuchinja ng’ombe nyumbani alikozaliwa na kula na wana Tandale huku siku ya Jumapili anatarajiwa kufanya sherehe kubwa na marafiki zake katika boti ya kifahari.