Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / ALIKIBA ASEMA WIMBO WAKE WA HELLA NI MAALUMU KWA MAREHEMU

ALIKIBA ASEMA WIMBO WAKE WA HELLA NI MAALUMU KWA MAREHEMU

| No comment
Related image

Msanii wa muziki na kipenzi cha wengi kutokea Kariakoo Dar es slaam, Ali Saleh Kiba, ameweka wazi sababu ya kudedicate wimbo wake mpya kwa dancer maarufu ambaye kwa sasa ni marehemu, Emanuel


Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Alikiba amesema marehemu Ima ndiye mtu ambaye alibuni style za kucheza kwenye wimbo huo na alikuwa akiupenda, na hata alipofariki aliwaahidi wenzake kuwa atauchia wimbo huo kwa heshima yake.


Image result for alikiba

“Nilliifanya nyimbo ya hela zamani sana kama 2013, sasa hivi nataka kuichaia kwa sababu dancer wangu Emmanuel ndiye aliitungia style ya kucheza akawafundisha wenzake wote, bahati mbaya Mungu alimpenda alifariki, na niliwaahidi dancers ambao walikuja kwenye msiba kwamba nitafanya nyimbo kwa sababu Ima alisimamia nyimbo ya hela kwa kiasi kikubwa sana, ahadi yangu nilitaka niitimize kwenye arobaini yake ambayo imepita hivi juzi”, amesema Alikiba.

Hata hivyo Alikiba amesema kwamba kwenye video ya wimbo huo ameweka picha za dancer huyo ambaye kwa sasa ni marehemu, kama kumpa heshima yake.