Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / WAZIRI PHILIP MPANGO KUWASILISHA BUNGENI MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA UBIA,SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFS

WAZIRI PHILIP MPANGO KUWASILISHA BUNGENI MUSWADA WA SHERIA YA MAREKEBISHO YA SHERIA YA UBIA,SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFS

| No comment

Waziri wa Fedha na mipango Mhe. Philip Mpango leo amewasilisha Bungeni muswada wa Sheria ya marekebisho ya Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.

Image result for philip mpango bungeni

Akisoma Bungeni lengo la mswada huu ni kufanya marekebisho ya Sheria ya Ubia ya Sekta Umma na Sekta Binafsi ili kuimarisha mfumo wa kitaasisi na kisheria katika usimamizi wa miradi ya Ubia na pia kutatua changamoto zilizopo katika utekelezaji wa miradi ya PPP (The Public Private Partinership (Amendment) Bill, 2018) ili kurahisisha uibaji, uidhinishaji na utekelezaji wa miradi ya PPP.

Vile vile muswada unakusudia kumpa Waziri mwenye dhamana na masuala ya fedha , mamlaka ya kusimamia utekelezaji wa sera, Sheria na kanuni za PPP kufuatia mabadiliko ya usimamizi wa programu ya PPP kupitia Hati ya Mgawanyo wa majukumu ya Mawaziri namba 114 ya mwaka 2016.

Madhumuni ya muswada huu ni kutatua changamoto mbalimbali zinazokwamisha utekelezaji wa programu ya PPP nchini ili kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia utaratibu wa PPP.