Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / WASANII WANAOFANYA VIZURI TANZANIA WANATOKA WCB! - BABU TALE

WASANII WANAOFANYA VIZURI TANZANIA WANATOKA WCB! - BABU TALE

| No comment

Image result for babu tale


Mmoja kati ya Wakurugenzi wa WCB, Babu Tale amefunguka kwa kudai kwamba kwa sasa wasanii ambao wanafanya vizuri nchini Tanzania wanatoka katika label yake ya WCB.

Akizungumza  Babu Tale alisema suala la mikataba ya wasanii wao lipo vizuri na hawana mpango wa kuipitia kama baadhi ya wadau wanavyoshauri baada ya kutokea sakata la Rich Mavoko.

“Hatuna mpango wa kupitia mikataba wa wasanii wa WCB, mikataba ya wasanii wetu wote haina matatizo, kama unavyoona wasanii wetu wote wanafanya vizuri,” alisema Babu Tale. “Wasanii wanaofanya vizuri nchini Tanzania kwa kipindi hichi wanatoka Wasafi iko wazi ukinuna ukiumia wasanii wanaofanya vizuri kwa kipindi hiki Wanatoka Wasafi,”