Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
NEWZ
'ULIMTUKANA RAIS JUKWAANI,MATENDO YAKO NDIO YEMEMUUA MAMA YAKO! AFANDE SELE
'ULIMTUKANA RAIS JUKWAANI,MATENDO YAKO NDIO YEMEMUUA MAMA YAKO! AFANDE SELE
Msanii mkongwe wa Hip Hop nchini Tanzania, Afande Sele amesema kuwa kwa upande wa vyama vya upinzani ni Professor Jay pekee ndiye Mbunge anayeonekana kufanya kazi kwa bidii huku akimtolewa mfano Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu kuwa anaendekeza siasa chafu za matusi jukwaani
Afande Sele amefunguka na kudai kuwa kauli ya Sugu kuwa mama yake amefariki kutokana na tukio la yeye kufungwa jela hilo ni kosa lake kwani alimtukana mkuu wa nchi, Rais Magufuli jukwaani jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mhe. Sugu wiki iliyopita Agosti 28, 2018 wakati wa kuuaga mwili wa marehemu mama yake jijini Dar es salaam, alisikika akisema kuwa mama yake alizidiwa zaidi na presha baada ya tukio la yeye kufungwa jela kwa kosa la kumtukana Rais Magufuli jukwaani, ambapo hadi mama yake anakufa alikuwa anaamini kuwa mtoto wake alifungwa kwa kuonewa jambo ambalo lilipelekea homa yake ipande.