Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / TCU IMEFUNGIA VYUO VIKUU VIWILI

TCU IMEFUNGIA VYUO VIKUU VIWILI

| No comment


TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imevifuta vyuo vikuu viwili kikiwemo cha Teofilo Kisanji (TEKU) cha Tabora na Mtakatifu Yohana (SJUT) cha Msalato, Dodoma, pia imesitisha utoaji wa mafunzo kwa vyuo vikuu 5 na kuamuru wanafunzi waliokuwa wanasoma vyuo hivyo kuhamishwa kabla ya kuanza muhula wa mwaka wa masomo 2018/19.


Hayo yamesemwa leo Septemba 25,2018 jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa ambapo amesema vyuo vilivyositishwa kutoa mafunzo ni; Chuo Kikuu cha Mlima Meru, Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga (ETU), Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta, Kituo cha Arusha (JKUAT- Arusha Center na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo) cha Bukoba mkoani Kagera.


“Vyuo hivi hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo kuanzia astashahada, stashahada (diploma), shahada (bachelor degree), shahada ya uzamili (masters) hadi shahada ya uzamivu (Phd) kwenye kozi yoyote ya masomo, vyuo hivi viko chini ya uangalizi maalum,” amesema.


Aidha, TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika kozi zote kwenye vyuo saba ambavyo ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian (MARUCo), Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kadinali Rugambwa (CARUMUCo), Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastina Kolowa (SEKOMU), Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania- Kituo cha Marko (SJUT- St. Mark’s Center) na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).


Mbali na hivyo, TCU imevitaka vyuo vikuu vyote vilivyotajwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo hayo na kwamba Tume inawaarifu wanafunzi wote wanaotakiwa kuhama kuwasiliana na vyuo vyao kwa ajili ya maelekezo kuhusu taratibu hizo.