Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
SOUDY BROWN KURUDISHWA MAABUSU
Kesi inayomkabili mtangazaji wa Clouds Media Soudy Brown, leo imesikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Peter Kibatala akisaidiana na Wakili Maghimbi.
Katika maelezo ya awali Soudy Brown anashtakiwa kwa kosa la kurusha maudhui kupitia akaunti yenye jina la Shilawadu ambayo haijasajiliwa
Baada ya Hakimu kusikiliza kesi hiyo upande wa utetezi umeomba mshtakiwa apewe dhamana ambapo Hakimu amekubali hivyo mshtakiwa ametakiwa kuwa na mdhamini mmoja na bondi ya shilingi milioni 2, kesi hiyo imeahirishwa hadi Octoba 18, 2018.
Hata hivyo, Soudy Brown bado anashikiliwa na amerudishwa tena polisi Central kwa kuwa ana kesi nyingine ya kujibu inayomhusu yeye pamoja na Msanii Maua Sama ambaye hakuletwa mahakamani leo.