Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUSIC NEWZ
"NATAKA MWANAUME MZUNGU" HAMISA MOBETTO
"NATAKA MWANAUME MZUNGU" HAMISA MOBETTO
Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka wazi mwanaume ambaye anataka kuishi naye kwa sasa, ambapo amedai kuwa anataka mwanaume wa kizungu ambaye alishawahi kuachika na mwenye watoto.
Akizungumzia vigezo vya mwanaume anayemtaka, Hamisa amesema kuwa kwa sasa hapendi kuolewa na vijana na anatafuta Mzungu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 45.
“Mimi hapa nataka labda mzungu au mtu mzima, awe alishawahi kuachwa au Mgane kwa hiyo ndio hivyo, yaani nikisema kijana dah hapana. Awe angalau miaka 45 kwa sababu mimi mwenyewe nina watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wangu,“amesema Hamisa Mobetto kupitia EATV.
Hamisa Mobetto tayari ameshazaa watoto wawili na wanaume wawili tofauti tofauti, ambao ni Diamond Platnumz na Majizzo na amesema kwa sasa hawezi kurudiana na yeyote kati yao
Kwa upande mwingine, Hamisa Mobetto amekiri kuwa sauti iliyosambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita akiongea na Mganga wa kienyeji ilikuwa ni ya kwake.