Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUSIC NEWZ
MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU WATUA KUIKABILI UGANDA
MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU WATUA KUIKABILI UGANDA
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Mbwana Samatta anayecheza katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji na mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Thomas Ulimwengu wametua nchini alfajiri ya leo.
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wametua nchini ili kujiunga na kambi ya timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Uganda.
Baadhi ya nyota wengine wanaocheza nje ya nchi na kuwasili ni Rashid Mandawa na Ramadhani Kessy.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Mandela uliyopo Namboole Uganda utakao fanyika Septemba 8 ya mwaka huu 2018.