Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUSIC NEWZ
MUNGU MKUBWA MAUA SAMA,SOUDY BROWN WAACHIWA KWA DHAMANA
MUNGU MKUBWA MAUA SAMA,SOUDY BROWN WAACHIWA KWA DHAMANA
Mtangazaji wa kipindi cha Shilawadu cha Clouds TV na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Maua Sama leo jioni ya Septemba 25, 2018 wameachiwa kwa dhamana ya jeshi la polisi.
Soudy Brown, Maua Sama na Meneja wake Fadhili Kondo wote wanatakiwa kesho kuripoti kituo cha kati (Central Police Station) saa 4 asubuhi.
Watatu hao jana walirudishwa mahabusu baada ya kupata dhamana ya kesi ya kwanza ya kuweka maudhui mitandao bila kibali kutoka kwa mamlaka husika, lakini waliendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa kile kilichodaiwa kuwa bado wanakosa lingine la kujibu, huku Mawakili wao wakizungumzia tukio la kukanyaga fedha ya Tanzania.