Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / MESSI AMPONGEZA RONALDO

MESSI AMPONGEZA RONALDO

| No comment

Mshindi wa tuzo ya Ballon d’or mara tano pia mchezaji wa FC Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusiana na uamuzi wa Mreno Cristiano Ronaldo kutimuka Real Madrid na kujiunga na mabibi kizee wa Turin Juventus.


Image result for messi na ronaldo

Messi amefunguka hayo wakati akiongea na kituo cha Radio cha Catalunya na kusema:-
“Real Madrid ni mojawapo ya timu bora sana duniani na wana kikosi kikubwa, lakini inaonekana kuwa wana ukosefu wa kujiamini bila Ronaldo kwani Ronaldo kuondoka kumewafanya kuwa duni na kuifanya Juventus kuwa mojawapo ya timu zinazotegemewa kushinda Ligi ya Mabingwa UEFA ”

Image result for messi na ronaldo

Messi aliongeza juu ya kuondoka kwa Ronaldo kutoka Santiago Bernabeu: “Nilishangaa sana na kunishtua alipoondoka Bernabu, Sikufikiria kuondoka Madrid na kujiunga na Juventus kwani Kulikuwa na timu nyingi zilizomtaka hicho ndio  kushangaa kwangu, lakini sio vibaya maana ameenda kwenye timu nzuri sana. ”

Image result for messi na ronaldo

Lakini pia akiongelea kuhusiana na mchezo wao wa El Clasco Messi alisema:- Anaamini Barcelona anaweza kuchukua faida ya kufanya vizuri dhidi ya wapinzani wao katika mchezo wa El Clasico kwani wapinzani wao hawana nguvu kama waliyokuwa nao, lakini pia anajua kuwa jitihada zote Ubingwa wa Ulaya unaweza ukatimukia huko Turin kwani kuna nguvu ya ziada imefanyika.
FC Barcelona wanaongoza ligi kuu nchini Uhispania kwa kuwa na alama 9 sawa na Real Madrid lakini wakiwa na tofauti ya magoli ya kufunga Barcelona akifunga goli 12 na kufungwa goli 2 huku Madrid wakifunga goli 10 na kufungwa goli 2.