Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / MC KOBA KUWAPA SIRI YA KURUDI KWENYE RAMANI WASANII WA ZAMANI

MC KOBA KUWAPA SIRI YA KURUDI KWENYE RAMANI WASANII WA ZAMANI

| No comment
Image result for KOBA MC

Mkali wa bongo fleva kutokea kundi la Watu pori, Koba mc amesema kuwa uwezekano wa wasanii waliowahi kufanya vizuri kwenye game ambao nafasi zao kama zimepotea hivi wanauwezo wa kurejea na kufanya vizuri tena endapo watakuwa mashabiki wa muziki wasasa na wasanii wanaofanya vizuri kujifunza kupitia wao.

"Mimi baada ya kuona kuna vita ya muziki hapa nyumbani niliamua kuwa shabiki wa wasanii tofauti na muziki wao ili kujifunza mbinu na namna ya uandishi wa sasa, hii imenisaidia kuendana na kasi ya muziki kwa sasa na hata wenzangu wanatakiwa kulikubali hili ili kurejea tena kwani muziki umekuwa mgumu na ushindani umekuwa" Alisema Koba.

Miaka ya hivi karibuni imekuwa ikiwapa wakati mgumu wasanii ambao walifanikiwa kuitengeneza mizizi ya bongo fleva kushindwa kufanya vizuri mbele ya damu changa. 

Koba ameachia kazi mpya "Umenuna" baada ya kipindi kirefu kupita bila kuachia kazi yoyote.