Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
GIGY MONEY KUPEWA ONYO LA MWISHO
Naibu Waziri ampa onyo la mwisho Gigy Money.
Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imempa onyo la mwisho msanii wa bongo fleva Gift Stanford maarufu kama Gigy Money kuachana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na endapo atakaidi tena amri hiyo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yake .
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.Juliana Shonza amesema kwamba hawata waangalia usoni wananchi pamoja na wasanii kiujumla watakao kuwa wanaenda kinyume na sheria ya mitandao.
"Huyu Gigy Money naona bado hajaacha michezo yake kwenye mitandao, safari hii sidhani kama atapona katika huu mchakato wa kuwakamata wasanii. Lakini kupona kwake labda yeye mwenyewe abadilike na awe kama hii sheria ya mitandao inavyotaka. Niwasii wasanii na watanzania wote kwamba waheshimu, mila na tamaduni za kitanzania kwasababu serikali ipo macho", alisema