Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / CHRIS BROWN ABURUZWA MAHAKAMANI NA MAMA MTOTO WAKE

CHRIS BROWN ABURUZWA MAHAKAMANI NA MAMA MTOTO WAKE

| No comment

Related imageChris brown aingia kwenye mgogoro wa kisheria na mama watoto wake, Nia Guzman.

Mtandao wa The blast umeripoti kuwa, Nia Guzman amefungua kesi Mahakamani chini ya mwanasheria Lisa Bloom akidai nyongeza ya pesa za matunzo ya mtoto wao, Royalty.

Kwa sasa Breezy anampa Nia kiasi cha $2,500 kwa mwezi na nyongeza ya $4,000 kwa ajili ya dada wa kazi na mlezi.

Nyaraka za mahakama zinasema, Nia ameiambia mahakama ya california kuwa pato la Breezy limeongezeka kwa miaka miwili iliyopita, akiingiza zaidi ya kiasi cha $4 milioni. Kwa mujibu wa sheria za usaidizi wa mtoto za mji huo, Nia Guzman anastahili kulipwa dola $21,000 kila mwezi sawa na Tsh. milioni 48.

Pato la mwezi kwa Breezy limetajwa kufikia $350.000 sawa na zaidi ya Tsh. milioni 800.