Shambulio hili lililofanywa na kikundi cha AL-QAEDA lilionesha udhaifu mkubwa wa ulinzi wa nchi ya MAREKANI kwa kuweza kushambulia majengo yao muhimu wakiwa humo humo ndani ya nchi yao kwa kutumia ndege za WAMAREKANI wenyewe.
Ukiona hivyo ujue ni shambulio la kutumia akili sana na nidhamu ya hali ya juu ili kuweza kuzizidi taasisi za usalama nchini humo ambazo zinafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha hakuna wa kuwadhuru ila kwa kwa shambulio hili walizidiwa kete na kuwa aibu kwa taifa kubwa kama MAREKANI kufanyiwa shambulio la namna ile.
KUZALIWA KWA WAZO LA SHAMBULIO
Turudi nyuma kidogo kuelekea kabla hatujafika kwenye kuzaliwa kwa wazo la shambulio la septemba 11,
Tarehe 25 disemba 1979 UMOJA WA KISOVIETI ulivamia nchi ya AFGHANISTAN kupambana na vikundi vya JIHAD vilivyokuwa vikisumbua serikali iliyoko madarakani ambayo ilikuwa ni mfuasi wa itikadi ya ujamaa.
Serikali hii ya AFGHANISTAN ilikuwa ni mshirika mkubwa wa UMOJA WA KISOVIETI na ilikuwa ikisaidiwa na taifa hili kiuchumi na kivita na ndo maana taifa hili kubwa likaamua kwenda kuvamia nchini humo ili kusaidia mshirika wake aweze kubaki madarakani na itikadi ya ujamaa iendelee.
Kipindi hiki kilikuwa bado ni kipindi cha vita baridi kati ya MAREKANI na washirika wake wa kibepari kama UINGEREZA, UFARANSA dhidi ya UMOJA WA KISOVIETI na washirika wake kama UJERUMANI MASHARIKI