Timu
ya Simba imekubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye
mchezo wa Ligi Kuu uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa leo Jumamosi.
Simba imekubali kupoteza mchezo huo muhimu ambao imetibua rekodi yao ya kutokufungwa mechi iliyoshuhudiwa na Rais John Magufuli.
Kagera
Sugar imekuwa timu ya kwanza kuvunja rekodi ya Simba ya kutopoteza
mchezo kwenye ligi msimu huu, ambapo mshambuliaji Okwi alikosa penati
iliyopanguliwa na Juma Kaseja na kushindwa kuinusuru timu hiyo.
Simba imekabidhiwa kombe la ubingwa la Ligi Kuu msimu wa 2017/18 na Rais John Magufuli.