ENGLAND: Klabu ya Soka ya Arsenal, kumtangaza Unai Emery kuwa Mwalimu mpya wa timu hiyo kuchukua mikoba ya Arsene Wenger aliyestaafu
-
Hapo awali uongozi wa Klabu ya Arsenal ulikuwa ukimpigia chapuo kocha msaidizi wa Manchester City, Mikel Arteta ambaye pia aliwahi kuwa mchezaji wa washika bunduki hao wa Jiji la London
-
Unai Emery mwenye umri wa miaka 46 amechaguliwa kukinoa kikosi hicho baada ya kuondoka kunako Klabu ya Paris St-Germain
-
Akiwa PSG alifanikiwa kunyakua ubingwa wa Ufaransa mara 1 na vikombe vinne vya ndani ya nchi hiyo katika kipindi cha miaka miwili,pia amekua kocha katika timu ya sevilla
