Hatimaye
yule mtanzania aliyesaidiwa kupata ufadhili wa matibabu na Mkuu wa mkoa
wa Dar es salaam, Mhe Paul Makonda amewasili leo hii majira ya saa 9:20
alasiri katika Uwanja wa kimataifa wa Beijing Capital. Mtanzania huyo
aitwaye Ahmed Albaity alipokekewa na Maafisa waandamizi wa ubalozi
pamoja na watanzania waishio hapa jijini Beijing na kusindikizwa kwenye
hospitali ya kimataifa ya Puhua.
Ndugu
Ahmed Albaity ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo
ambalo limedumu kwa takribani miaka kumi na moja akiwa kitandani,tayari
ameanza kupatiwa Matibabu katika hatua za awali mara tu baada ya
kuwasili hospitalini hapo.
Mapema
akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi wakitanzania Wanaosoma na kuishi
nchini humo Bw. Remidius Emmanuel ambaye pia ni Katibu Mkuu Shirikisho
hilo amesema wao kama watanzania wanaosoma na kuishi katika Taifa la
China wameshiriki kumpokea Mtanzania mwenzao (Ndugu. Ahmed Albaity )
na kwamba kwa kipindi chote ambacho atakuwepo hapa Beijing China
wataendelea kutoa Ushirikiano na kumjulia hali wakati wote.
"Tunamshukuru Mwenyezi MUNGU amemuongoza Bw.Ahmed kufika salama hapa Beijing, Tumeshuhudia watanzania wakimsindikiza uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda, huu ni upendo wa kipekee, na sisi tumeguswa na kuwiwa kumpokea tukiongozwa na Maafisa waandamizi wa Ubalozi wetu hapa China" Alisema Bw. Remidius.
Kwa
upande wake ndugu Ahmed Albaity ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini
China pamoja na uwakilishi wa Watanzania wanaosoma na kuishi nchini humo
kwa moyo wao wa upendo na namna walivyoweza kumpokea yeye na ujumbe
alioambatana nao.
Bw.Michael
Semindu moja kati watanzania wanaosoma nchini humo aliyeshiriki
mapokezi hayo alimhakikishia Ndugu Ahmed Ushirikiano kwa kipindi chote
atakachokuwa kwenye matibabu jijini Beijing "Nimefurahi kuungana na
Maafisa wa Ubalozi pamoja na watanzania wenzangu kumpokea mwenzetu,
tunamuahidi ushirikiano kwa kipindi chote atakachoendelea kupata
matibabu nchini China" Alisema Bw. Michael