Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Serikali yamnyang’anya shamba Manji

Serikali yamnyang’anya shamba Manji

| No comment

Serikali imelifuta shamba la mfanyabiashara Yusuf Manji, lenye ukubwa wa eka 714 kigamboni.


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema leo Jumatano kuwa, shamba hilo litapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amesema shamba lingine la kampuni ya Amadori lenye ukubwa wa eka 5,400 pia limefutwa.

Waziri amesema mashamba hayo sasa yako mikononi mwa Serikali na yatapangiwa matumizi mengine.

Lukuvi amewaonya wananchi wasivamie maeneo hayo kwa kuwa watakaokamatwa  watashitakiwa.

"Muyaache maeneo hayo kama yalivyo mkijenga tutakuja kuvunja," amesema.