Wimbo mpya wa rapa Darassa, Hasara Roho unaendelea kuchanja mbuga kupitia mitandao ya kijamii ambapo mpaka sasa kwa kipindi cha mwezi mmoja wimbo huo kupitia mtandao wa YouTube umeshaangaliwa mara 1,617,942.

Hii ni hatua nzuri kwa rapa huyo ambaye wimbo wake uliopita ‘Muziki’ umeweza kufikisha views 8,433,300 kwa kipindi cha miezi 6.
Akiongea na Bongo5 hivi karibuni meneja wa rapa huyo, Hanscana, alidai kila wimbo ambao utakuwa unatoka kwa rapa huyo utakiwa ni nzuri na wenye kuleta ushindani kwa nyimbo nyingine.
“Sisi tunaandaa kazi zakutosha na kazi ambazo kila moja ikitoka utasema hii ni kazi zaidi ya iliyopita,” alisema Hanscana.
Maswali kwa mashakini ni kutaka kujua kama wimbo huo mpya Darassa kama unaweza kuvunja rekodi iliyoandikwa na muziki.