Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
BETRI INAYOZALISHA UMEME KWA ALMASI NA TAKATAKA YA NYUKLIA
Chuo Kikuu cha Bristol cha Uingereza kimeonesha betri inayozalisha umeme kwa almasi na takataka za nyuklia. Lakini teknolojia hii bado iko kwenye kipindi cha majaribio na matatizo mbalimbali bado hayajatatuliwa.
Watafiti wameweka rasilimali inayotoa mionzi ndani ya almasi iliyotengenezwa na binadamu ili kuzuia mionzi isivuje nje. Sasa wametumia rasilimali inayotoa mionzi ya Nickel-63 kutengeneza betri hii, lakini wanaendelea kufanya majaribio kwa kutumia rasilimali ya Carbon-14 ili kuongeza ufanisi wa kuzalisha umeme. Kwa nadharia watu wataweza kukusanya Carbon-14 kutoka kwenye takataka za nyuklia.
Dk. Neil Fox amesema ni hatari kwa ngozi ya binadamu kuvuta mionzi inayotoka kwenye Carbon-14, lakini almasi ni kitu kigumu zaidi kinachoweza kuwalinda watu kutodhuriwa na mionzi.
Tatizo la sasa ni kwamba ni vigumu kutengeneza betri hiyo na gharama ya kuitengeneza ni kubwa, lakini jambo zuri ni kwamba betri hii haileti uchafuzi mwingine na inaweza kufanya kazi kwa zaidi ya miaka elfu moja.
Related Posts
- Default comments
- Facebook comments
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
.
Popular Posts
-
Tofauti na watu wengi wanavyodhani, kizunguzungu huwa ni ishara ya tahadhari inayotolewa na mwili kuwa kuna kitu hakiko sawa, hivyo uchung...



