Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / M2 The P kuachia albamu mpya

M2 The P kuachia albamu mpya

| No comment
Msanii wa muziki,M2 The P anajipanga kuachia albamu yake mpya ambayo amedai itakuwa na kolabo nyingi zaidi.
m2thep
Akiongea na Bongo5 wiki hii, M2 The P amesema hana sababu ya kuendelea kuogopa kutoa albamu kutokana na soko lilivyo.
“Kuna mambo mengi mazuri yanakuja tukiachana na project yangu na Mirror na Jodan, kuna project mpya mimi na Mr Blue inakuja. Wimbo unaitwa ‘Nakuonga’ ambapo pia utakuwa kwenye albamu yangu ambayo nitaichia soon Mungu akipenda,” alisema M2 The P.
Aliongeza, “Albamu ni CV ya msanii, msanii ukiwa na albamu kuna uzito fulani ambao unakuwa nao tofauti na wasanii wengine, kwa hiyo albamu yangu itakuwa na kolabo nyingi ili kupata ladha ya wanamuziki tofauti tofauti,”
Pia muimbaji huyo amewataka wasanii wenzake kutoa albamu kwa wingi huku akidai soko la albamu litajitengeneza taratibu.