Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Serengeti Boys kuweka kambi ya siku 9 Shelisheli

Serengeti Boys kuweka kambi ya siku 9 Shelisheli

| No comment
Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys inatarajia kuondoka Jumapili ya Septemba 4 mwaka huu kuelekea visiwa vya Shelisheli katika kambi ya siku tisa ya maandalizi ya mchezo wa mwisho dhidi ya Congo-Brazaville
Serengeti Boys
Mchezo huo ni kwa ajili kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana yanayotarajiwa kufanyika mwakani nchini Madagascar.
Mwenyekiti wa kamati ya soka la vijana Ayubu Nyenzi amesema, timu inaendelea na mazoezi chini ya kocha Bakari Shime ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya awali wakitokea katika mapumziko mara baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Amajimbos ya Afrika kusini.
Nyenzi amesema, anaamini maandalizi hayo yataiwezesha timu hiyo kuweza kusonga mbele na kuweza kufanya vizuri katika mashindano ya fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana.
Nyenzi amesema, wameshaanza kuwafuatilia wapinzani wao ikiwa ni sehemu ya kuangalia ni jinsi gani wapambane ili kuweza kujihakikishia wanaweza kusonga mbele katika mashindano hayo.