Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Rais Magufuli kuwasili Lusaka, Zambia kesho kwa ziara ya siku tatu

Rais Magufuli kuwasili Lusaka, Zambia kesho kwa ziara ya siku tatu

| No comment
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho  Septemba 12 2016 anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia.
Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika kesho kutwa tarehe September 13 2016 katika Jiji la Lusaka. Rais Magufuli anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Kamati hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.
Dkt. Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne Jamhuri ya Msumbiji Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.
Katika Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Lusaka