Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / OLIVER MTUKUDZI SIMBA WA AFRIKA ANGURUMAE MAWINDONI

OLIVER MTUKUDZI SIMBA WA AFRIKA ANGURUMAE MAWINDONI

| No comment
Yatosha

Shabiki yeyote wa muziki ukitajwa wimbo wa Wasakara amaNdakuvara pasi na shaka tunasomana vizuri lakini kama wewe ni kizazi cha .com bado hujachelewa saaaaana kwani wimbo maarufu wa Todiiama Neria sio mgeni sana masikioni mwako kwa kuwa vibao hivi vimefanywa na nguli mashuhuri nchini Zimbabwe Oliver Mtukudzi maarufu kama Tuku vikatamba sana Afrika na kupata mashabiki wengi.oliver-mtukudzi

Oliver Mtukudzi alianza muziki miaka 39 iliyopita ambapo hadi sasa amefanikiwa kutoa albamu 65 zinazomfanya hadi leo atambulike na kupewa heshima kubwa na nchi mbalimbali barani Afrika na ulimwenguni.

Mtukudzi anatarajia kuzindua rasmi albamu yake ijulikanayo kama Eheka! Nhai Yahwe usiku wa leo akisindikizwa na wasanii kama Jah Prayzah, Tariro neGitare na Sam Dondo.oliver-mtukudzi

Nimuonavyo  Tuku ni kama simba aliyepo mawindoni anayepita huku na huko akinguruma kutafuta kitoweo bila kuchoka kwani licha ya kuwa na umri mkubwa na kufanya muziki kwa kipindi kirefu nguli huyu bado ameendelea kuonesha shauku yake ya kufanya muziki unaoendelea kumpa heshima duniani kote siku hadi siku.