Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / MTV MAMA 2016 MWAKA WA DIAMOND, KIBA NA NAVY KENZO

MTV MAMA 2016 MWAKA WA DIAMOND, KIBA NA NAVY KENZO

| No comment

Image result for alikiba and diamond platnumzHatimaye vipengele vya Tuzo za MTV Mama kwa mwaka 2016 vimewekwa hadharani huku wasanii 3 kutoka Tanzania wakitangazwa kuwania tuzo hizo katika baadhi ya vipengele. Katika vipengele hivyo vipatavyo 8 nchi ya Tanzania inawakilishwa na wasanii Diamond Platnumz, Ali Kiba pamoja na Kundi la Navy Kenzo.

MTV 2016MTV 2016

Tuzo hizo zenye heshima kubwa sana barani Afrika zinatarajiwa kufanyika nchini Afrika Kusini Jumamosi ya Oktoba 22 mwaka huu  zikiwahusisha pia wasanii nyota wa ndani na nje ya Afrika kuchuana kutwaa tuzo hizo.

Diamond Platnumz ambaye anashiriki kwa mara ya nne mwaka huu akifanya hivyo mwaka 2010 alipokuwa kwenye vipengele 2, ‘best new artist’ na ‘best male’ lakini hakufanikiwa kuchukua tuzo, mwaka 2014 tena alifanikiwa kuchaguliwa kwenye tuzo hizi wakati huo akiwa kwenye kipengele kimoja tu cha ‘best collaboration’ kwenye wimbo wa ‘my number one remix’ alioshirikiana na Davido hata hivyo haukuweza kunyakua tuzo hiyo. Mwaka 2015 ulikuwa wa bahati sana kwake mara baada ya kunyakua tuzo moja kati ya  alizokuwa akiwania, akiwekwa kwenye vipengele 3 ‘best male’ ‘best collaboration’ na ‘best live act’ ambacho kilimpa tuzo. Mwaka huu yupo katika kipengele kimoja tu cha ‘best male’ ambapo anagombea tuzo hizi na wakali kibao kama, Black Coffee wa South Africa, AKA wa South Africa, Wiz Kid pamoja na Patoranking wote wa Nigeria.

diamonddiamond

Wawakilishi wengine wa Tanzania katika tuzo hizi, ni kundi la Navy Kenzo wenyewe hii ni mara yao ya kwanza kuingia kwenye tuzo hizi lakini wakichagizwa na vibao vyao vilivyofanya vizuri sana kwenye bara la Afrika kama ‘game’ walioshirikiana na Vanessa Mdee pamoja na ‘Kamatia’ ambao umefanya vizuri sana kwenye vituo mbalimbali vya radio na tv barani Afrika wapo tayari kupambana kwenye kipengele cha ‘best group’ ambapo watachuana vikali na makundi mengine kama ‘Toofan’ kutoka Togo, ‘Micasa’ South Africa pamoja na ‘R2Bees’ kutoka Ghana.

navy KENZOnavy KENZO

Ali Kiba ni msanii mwingine kutoka Tanzania ambaye licha ya kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye tamasha hilo, pia atawania tuzo ya wimbo bora wa kushirikiana ‘best collaboration’ kupitia wimbo alioshirikishwa na kundi la Sauti Sol uitwao ‘Unconditionally Bae’.

SAUTI SOLSAUTI SOL

Ni wakati wa Watanzania sasa kuwapa sapoti wasanii wetu hawa kwa kuwapigia kura kwa wingi ili watuwakilishe vyema kwa kuleta tuzo hizi nyumbani