Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Michuano ya Judo Taifa kuanza Novemba 19, Dar

Michuano ya Judo Taifa kuanza Novemba 19, Dar

| No comment

Mashindano ya Kitaifa ya mchezo wa judo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 19 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa kushirikisha vilabu mbalimbali hapa nchini.
Katibu Mkuu wa Chama cha Judo nchini JATA Innocent Malya amesema, wameshatuma barua kwa vilabu vyote nchini ili kuweza kupata vilabu vingi zaidi ambavyo vitatoa wachezaji wa timu ya taifa watakaoshiriki mashindano ya kanda ya tano yanayotarajiwa kufanyika Februari 02 mwakani visiwani Zanzibar.
Malya amesema, wamevitaka vilabu vyote ambavyo vitahitaji kushiriki kuhakiki mapema ili kuweza kutoa nafasi kwa chama kupanga ratiba mapema ambapo mwishoni mwa kuhakiki ushiriki wa mashindano hayo ni Novemba 12 mwaka huu.