Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / MFUMO MPYA: Jipange kuingia uwanja wa taifa kwa kadi na sio cash tena

MFUMO MPYA: Jipange kuingia uwanja wa taifa kwa kadi na sio cash tena

| No comment
Jumapili Septemba 11 2016 waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauye kwa niaba ya waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa amezindua rasmi matumizi ya tiketi za kielektroniki katika uwanja mkuu wa taifa.
img_0159
Mfumo huo ni agizo la waziri mkuu Majaliwa kuhusu udhibiti wa mapato kwenye viingilio vya mlangoni ambapo ni mfumo utakaomtaka shabiki kuwa na kadi mfano wa zile za ATMambapo atakuwa na uwezo wa kadi yake aliyopewa kufanya manunuzi/malipo akiwa pia na uwezo kununua tiketi za mechi atazopenda kupitia kadi hiyohiyo.
img_0163
Miongoni mwa waliopewa kadi za kuingilia uwanjani ni waziri Nape, Rais Magufuli na makamu wake mama Samia Suluhu ikiwa ni uhamasishaji ambapo smartcard hiyo ya kukuwezesha kuingia uwanjani itatolewa bure kwa shabiki na baada ya hapo ataanza kuingia nayo uwanjani baada ya kuiwekea pesa.
img_0173
Faida nyingine ya mfumo huo ni kuwa hakutakuwa tena na utaratibu wa kugawanya mapato kwa njia ya mkono kwenda katika taasisi husika ila ukikata tiketi asilimia za mgawanyo zitakuwa zinafanywa kiteknolojia zaidi kwenda TFF, TRA, BMT na sehemu nyingine zinazohusika