Msanii Mataluma ambaye alitamba sana kwa miondoko ya mchiriku kwa ngoma yake ya Kariakoo, amedhamiria kurudi kwenye game kwa madai ya biashara zake kwenda kombo.Msanii Mataluma ambaye alitamba sana kwa miondoko ya mchiriku kwa ngoma yake ya Kariakoo, amedhamiria kurudi kwenye game kwa madai ya biashara zake kwenda kombo.
Mataluma
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Mataluma amesema alipokuwa kimya kwenyegame alikuwa anafanya biashara ya mkaa, lakini kutokana na mfumo mpya kuwa mgumu ameamua kurudi kwenye game kwani muziki anaona unalipa kwa sasa kuliko biashara ya mkaa akliyokuwa akifanya.
"Nilianza muda mrefu kwenye mkaa nikawa kimya watu hawanisikii, lakini kutokana na serikali kuamua kutaka vibali na nini, ndo nimeamua sasa hivi kutulia na kurudi kwa nguvu zangu zote kwenye muziki, kwa sababu muziki ninauweza na naona sasa hivi muziki sasa hivi unalipa kuliko hata huo mkaa", alisema Mataluma.
Mataluma aliendelea kuweka wazi kuwa kutokana muziki wa singeli kwa sasa kufanya poa zaidi, na yeye alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa muziki huo, hatarudi kwenye singeli bali atafanya mchiriku, ili kuweka utofauti kwenye game.
"Waanzilishi wa singeli, waanzilishi wa mchiriku mimi ndo wa kwanza kufanya nao kwa sababu hii bongo fleva unayoisikia mi ndo mtu wa kwanza kuimba na Manfongo na Msaga Sumu, mi ndo wa kwanza kwa hiyo wasione ajabu na mimi niko vizuri, sijaamua kuzitoa hizo kazi ingawa naweza, lakini si kwenye muziki wangu wa mara ya kwanza Mama mubaya na Kariakoo, mi niwaachie kisingeli mi nifanye mchiriku", alisema Mataluma.