Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa atahamia rasmi mjini Dodoma hii leo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa sikukuu ya mashujaa Julai 25 Mwaka huu.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
Taarifa iliyotolewa na Ofisa Uhusiano na Mawasiliano wa Mkoa wa Dodoma, Jeremiah Mwakyoma kwa vyombo vya habari imesema maandalizi ya mapokezi yamekamilika.
Mwakyoma amesema Majaliwa atawasili mjini Dodoma katika uwanja wa ndege wa Dodoma mchana na atakuwa na ziara ya siku mbili kukagua hatua za maandalizi ya ujio wa serikali mjini humo.