Producer Lamar amedai kuwa hadi sasa pengo la marehemu Geez Mabovu ni kubwa na anaendelea kulihisi.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Vibe la Kitaa cha ABM Radio ya Dodoma, DJ Rodger, Lamar amesema Geez alikuwa zaidi ya msanii kwake.
“Geez Mabovu nilifanya naye kazi tangu naanza career yangu, nimekutana naye nikiwa G Records kuanzia mwaka 2004 ingawa nilikuwa namsikia kipindi cha nyuma, lakini kuanza kufanya kazi tulianza 2006 Bongo Records,” alisema Lamar.
“Geez toka amefariki kuna vitu vingi ambavyo navimiss kutokana na Geez hakuwa sio artist kwangu, alikuwa kama ndugu yangu, mtu ambaye alikuwa close na mimi, tunashare vitu vingi halafu kwao wananijua home kwetu alikuwa anakuja kama nyumbani. Mpaka sasa hivi baba yake nawasiliana naye,” ameongeza.
“Mwaka jana nilienda kwao kwenda kutembelea mpaka kaburi lake, kwahiyo kuna vitu vingi ambavyo nimevimiss kutoka kwa Geez.”
Lamar amesema rapper huyo aliacha album yenye nyimbo takriban 10 na kwamba anasubiria muda muafaka wa kuachia single ya kwanza.
Geez alifariki November 2014