Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / JIKO LAUA WATATU WA FAMILIA MOJA

JIKO LAUA WATATU WA FAMILIA MOJA

| No comment

WATU watatu wa familia moja wamefariki dunia, huku mmoja akikimbizwa hospitalini, katika kijiji cha Lualaje, kata ya Kipembawe, wilayani Chunya, kutokana na kukosa hewa ya Oxygen baada ya kulala ndani huku wakiwa wameacha jiko la mkaa likiwaka.

Akitoa taarifa ya tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Rehema Madusa, aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni baba wa familia hiyo, Leonard Mwashambwa (42) na watoto wake wawili ambao ni Mponeje Leonard mwenye umri wa miaka mitatu na Zaituni Leonard wa mwaka mmoja.

Alisema mama wa familia, Rhoda Darama (22) alikutwa amepoteza fahamu na kwamba alikimbizwa katika hospitali ya wilaya hiyo, ambako alipatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Tukio hilo lilibainika baada ya majirani wa marehemu kuamka asubuhi na kuona milango ya nyumba hiyo haifunguliwi na kuamua kuita kwa ajili ya kuwajulia hali majirani zao hao lakini bila mafanikio.