Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Bodi ya hakimiliki Kenya yazifurahia EATV AWARDS

Bodi ya hakimiliki Kenya yazifurahia EATV AWARDS

| No comment
Bodi ya Hakimiliki ya Kazi za Sanaa nchini Kenya (MCSK), imeipa baraka zake EATV AWARDS huku ikisema ni jambo jema kwenye tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki kuwepo kwa tuzo hizo.
Akizungumza na East Africa Television, kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo Merit Simiyu, amesema hilo ni jambo jema kwa wasanii kwani litatoa fursa kwa wasanii wa nchi hizo kujulikana kwenye nchi nyingine pamoja na kazi zao.
"Itakuwa vyema sababu wasanii wote ni familia moja, na ikiwa wataweza kuwa na ile 'platform' ya kuwa na event kama hii, naona sisi kama wasimamizi wa wasanii nchini Kenya hatuna shida tutaweza kuisapoti, sababu sisi tupo hapa tuweze kushughulikia wasanii waweze kuimarika, na tuzo kama hizi ndio njia moja inayofanya wasanii wengine ambao hata hawajulikani, waweze pia kujulikana Afrika Mashariki,"alisema Merit Simiyu ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa bodi hiyo.
Bwana Simiyu aliendelea kusema kuwa wao kama bodi inayosimamia wasanii watatoa idhini kwa wasanii kushiriki kwenye tuzo hizo,
"Hivi sasa tuko na wasanii elfu 15 ambao wamejisajili, na hiyo ni idadi kubwa sababu wasanii wako na imani na chama chetu (MCSK), sisi tutawapa idhini kwa wasanii wote ambao wamechaguliwa au wanaotaka kushiriki, ili waweze kushiriki hatuna shida”, alisema Merit Simiyu.