Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Nisamehe’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha AliKiba, amesema katika interview yake kubwa iliyopita na MTV aliomba kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha ambayo anaweza kuizungumza.
“Niliulizwa kwenye interview ya MTV kama naweza kuongea kingereza, nilichowajibu naweza ila sio Kingereza kilichonyooka ndio maana nikatumia Kiswahili. Nafurahi kwa kuwa walivutiwa na kiswahili,” Barakah alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM Jumanne hii.
Pia muimbaji huyo amesema mpenzi wake wa sasa Naj ameshindwa kufundisha kuhu akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu.
“Hanifundishi lugha kwa sababu tuna masihala mengi hivyo nahitaji mtu ambae atakuwa serious,” alisema Barakah.
Diamond ni miongoni kati ya wasanii ambao walikuwa hawajaui kuongea lugha ya Kigereza lakini alijifunza na sasa anakichapa kama kawaida