Unaikumbuka Masebene? Ni ngoma ya aliyekuwa msanii chipukizi zaidi ya miaka miwili iliyopita, Y-Tony hadi kumpa nomination kwenye tuzo za Kili.
Kwa sasa amekua, amejifunza, ameiva na amerejea tena na kigongo kipya ‘Wivu Wangu’ shukrani kwa mipango mikubwa iliyonayo kampuni mpya inayomsimamia kwa sasa, Fresh Code Entertainment King
hivyo ujio wake mpya si wa single tu bali maandalizi makubwa ya kuja kabisa na album na tayari amesharekodi ngoma kibao.
Akiongea na kipindi cha Extra Fleva cha Uplands FM kinachosimamiwa na mtangazaji Ergon Elly, Tony ambaye jina lake halisi ni Elly Michael Kilema, amesema jina na tarehe ya kuachia album hiyo anauachia uongozi wake na kwamba pindi ambapo kila kitu kitakuwa kimekamilika, vitawekwa wazi.