Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Waziri Nape kuvifungia vituo vya Radio 5 na Magic Fm

Waziri Nape kuvifungia vituo vya Radio 5 na Magic Fm

| No comment
August 29 2016 Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Nape Nnauyeametangaza kuvifungia vituo viwili vya radio kwa muda usiojulikana ambavyo ni Magic Fm ya Dar es salaam na Radio 5 ya Arusha kwa makosa ya kutangaza na kutoa habari za kichochezi.
Waziri Nape amesema…>>>’Nimevifungia vituo viwili vya radio ambavyo ni Radio 5 Arusha na Magic Fm Dar kwa muda usiojulikana kwa kosa la uchochezi, hadi sasa nimeelekeza kamati ya maudhui kuviita vyombo hivyo na kuwasikiliza kwa kina kisha kunishauri hatua zaidi ya kuchukua
Adhabu hii ya kuvifungia kwa muda vituo hivyo viwili inaanza leo August 29 2016 hadi pale kamati itakapomaliza kazi yake, kimsingi radio zote mbili kwa pamoja wametangaza na kutoa habari ambazo zina uchochezi ndani yake‘ –Waziri Nape