Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / WAZIRI MKUU MH MAJALIWA AMESEMA HAYA KUHUSU SUKARI NCHINI

WAZIRI MKUU MH MAJALIWA AMESEMA HAYA KUHUSU SUKARI NCHINI

| No comment

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amevitaka viwanda vya sukari nchini kuongeza mikakati ya uzalishaji zaidi ili mwaka 2020 Tanzania iwe imefikia kiwango cha kuzalisha asilimia 100 ya mahitaji yake.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo  wakati alipotembelea kiwanda cha sukari cha Mtibwa kilichoko mkoani Morogoro ambapo amesisitiza viwanda vya ndani vizalishe zaidi ili kupunguza uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi.

Image result for sukari tanzania

Amesema Serikali imejikita katika kuimarisha na kulinda viwanda vya ndani nchini hivyo ni vema viwanda vya sukari vikaweka mikakati ya kuzalisha kwa wingi ili kuondokana na uagizaji wa bidhaa hiyo kutoka nje.

“Kiwango cha mahitaji ya sukari nchini ni zaidi ya tani 400,000, nimeiagiza Bodi ya Sukari kukaa na wataalamu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na kufanya utafiti ili tujue mahitaji halisi ya sukari,” alisema.