Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / VYUO VITANO VYA FUNGIWA NA NACTE.

VYUO VITANO VYA FUNGIWA NA NACTE.

| No comment

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, NACTE, limevifuna vyuo 5 kutokana na kukiuka taratibu na vyenye mapungufu makubwa ya usajili na ithibati

Akiongea na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa ,NACTE, Mhandisi Steven Mlote, amesema Baraza limetoa muda wa mwezi mmoja kwa vyuo 112 kutekeleza masharti ya usajili na vyuo 52 kutekeleza masharti ya ithibati kwa mujibu wa sheria za uendeshaji vyuo vya ufundi nchini, na vyuo vitakavyoshindwa kutekeleza agizo hili vitafungiwa mara moja.Vyuo vilivyofungiwa nipamoja na State College of Health and Allied Aciences cha Dar es salaam, Zoom Polytechnic College cha Dar es salaam, Thabitha College – Dar es salaam formerly Thabita Voccational Training College cha Dar es salaam, Financial Training Centre cha Dar es salaam na TMBI College of Bisiness and Finance cha Dar es salaam.

Mhandisi Mlote ametolea mfano chuo cha State Colege of Health and Allied Sciences cha Dar es salaam kuwa huwa kama chuo mchana wakati nyakati za usiku ni klabu ya pombe hivyo mazingira yake kutofaa kwaajili ya kufundishia.