Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / SIMBA KUVUNA MILIONI 130 ZA USAJILI WA KESSY KUTOKA YANGA

SIMBA KUVUNA MILIONI 130 ZA USAJILI WA KESSY KUTOKA YANGA

| No comment

SIMBA imewasilisha barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka Yanga iwalipe dola za Marekani 60,000 (sawa na Sh milioni 130) kwa madai ya kumsajili mchezaji Hassan Kessy kinyume na taratibu.

Kesi ya madai ya Simba dhidi ya Yanga inatarajiwa kunguruma Jumamosi ya wiki hii pale Kamati ya Sheria na Hadhi kwa wachezaji chini ya Mwenyekiti wake Richard Sinamtwa itakapokutana.KESSIKaimu Mkurugenzi msaidizi wa Sheria na uanachama wa TFF, Eliud Mvela alisema jana kuwa Simba imewasilisha barua ya madai kwa Shirikisho hilo juzi na hivyo Jumamosi kesi hiyo itatolewa ufumbuzi.

Kessy, hivi karibuni alishindwa kuitumikia Yanga katika mashindano ya kimataifa kutokana na Simba kugoma kutoa barua ya kuthibitisha kumalizana na beki huyo kwa madai kuwa alikiuka makubaliano kwa kusaini mkataba mwingine kabla ya aliokuwa nao kumalizika.