Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa nchini Afrika Kusini

Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa nchini Afrika Kusini

| No comment
Moi-Kibaki.Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.
Moi-Kibaki
Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.
“Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka,” taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.
Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.
Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.
Mkewe, Lucy Muthoni Kibaki, alifariki Aprili mwaka huu akitibiwa jijini London.
Source: BBC