Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
Siasa
POSHO KUGHARAMIA SAFARI YA DODOMA
POSHO KUGHARAMIA SAFARI YA DODOMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama amesema suala la bajeti ya kuhamishia makao makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam litatatuliwa kwa kutumia posho za safari za mawaziri.
Akizungumza katika kipindi cha Safari ya Dodoma kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mhagama amesema suala la bajeti wanalijua wenyewe serikalini.
“Bajeti tulizopanga, hasa ya 2016/17 sisi tunajua tulipanga nini, tunafahamu mapato yaliyopitishwa na Bunge yakoje. Kwa mfano mimi Jenista (waziri) kwa mwaka huu mzima wa fedha nina mikutano minne Dodoma.
Kwenye ile mikutano yote natakiwa kulipwa posho, maana yake ni kuwa napaswa nipate posho ya miezi mitano, sasa fedha hiyo ndiyo itakayoingizwa kwenye gharama za kuihamishia Serikali Dodoma,” amesema.