Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / PAMOJA NA ELIMU BURE,WANAFUNZI 10,273 HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA

PAMOJA NA ELIMU BURE,WANAFUNZI 10,273 HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA

| No comment
Image result for wanafunzi wa primary

Ukaguzi uliofanywa na Wizara ya Elimu katika shule 6,831 za msingi mwaka 2015/16 umebaini kuwepo kwa wanafunzi 10,273 wasiojuajua kusoma wala kuandika.

Jambo hilo limeilazimu Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kutoa mafunzo kwa wadhibiti ubora wa shule 1,469 ili kuondoa tatizo la wanafunzi wanaomaliza shule wakiwa awajui kusoma wala kuandika.

Akiongea  jijini Dar es salaam Jijini Dar es salaam , Mkurugenzi wa Idara ya ya udhibiti Ubora wa Shule Bi. Merisela Wasena amesema baada ya kufanya utafiti katika shule za msingi 6,831 wamebaini idadi hiyo ya wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika katika shule 515 huku wasichana wakiwa ni 5, 263 na wavulana ni 5010.

Merisela amesema, hatua ya sasa imechukuliwa kupitia mpango wa ufundishaji na ujifunzaji wa kusoma, kuandika na kuhesabu KKK chini ya mtaala wa shule za msingi kwa darasa la kwanza na darasa la pili litawawezesha wanafunzi kufika darasa la nne wakiwa wanajua kusoma na kuandika hivyo kuondoa changamoto hiyo wafikapo darasa la saba.