Mr Blue amekiri kuwa skendo yake kuwa amekuwa akiwasiliana na ex wake, Naj ambaye kwa sasa ana uhusiano na Barakah Da Prince ilitaka kuivunja ndoa

Akiongea na Clouds FM, rapper huyo wa ‘Mboga Saba’ amedai kuwa mke wake, Wahyda sasa amekuwa na wivu wa kufa mtu tangu kuzuke skendo hiyo.
“Sasa hivi naona kama wivu umezidi baada ya hii skendo ya hawa jamaa kuitengenezea kiki kwasababu wanataka kutoa nyimbo yao, skendo kwamba mimi nilimpigia yule mwanamke mwingine nani anaitwa, Najma yule. Wametengeneza kweli kabisa, mimi nimezipata za kunyapianyapia kwamba wametengeneza ili kukikisha nyimbo zao,” amesema Blue.