MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Biashara imeamuru Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi afike mahakamani kujieleza kwa nini asifungwe gerezani kwa kushindwa kutekeleza hukumu inayohusu malipo ya Sh bilioni 1.2.
Mengi anatakiwa kufika mahakamani hapo Agosti 24, mwaka huu kujieleza kutokana na kushindwa kutekeleza hukumu iliyomtaka kuwalipa wafanyabiashara watatu, Muganyizi Lutagwaba, Eric Mshauri na Charles Mgweo, Dola za Marekani 598,750 sawa na Sh bilioni 1.2.
Alitakiwa kuwalipa fedha hizo kutokana na mgogoro wa malipo ya uuzwaji wa hisa katika Kampuni ya Douglas Lake Minerals Ltd ambayo kwa sasa inaitwa Handeni Gold Inc.