Akiongea na kipindi cha Extra Fleva kinachoendeshwa na mtangazaji Ergon Elly, member wa kundi hilo, Kay alidai kuwa album hiyo itazungumzia maisha ya ghetto. Amedai kuwa katika maisha ya ghetto wengi wanapitia changamoto, furaha, huzuni huku pia wakitakiwa kuwa na uvumilivu.
Album hiyo itaingia sokoni Jumatano hii siku yao ya kuzaliwa na itakuwa na jumla ya nyimbo 10.
Wasanii walioshirikishwa kwenye Ghetto Love ni pamoja na Mansu Li,Nikki Mbishi,Saraha, Damian Soul na wengine huku watayarishaji wakiwa ni pamoja na Fundi Samweli, DX wa Noiz Maker na wengine.