Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / MAJIBU YA TALE BAADA YA WASANII WA WCB KUTOTAJWA KWENYE FIESTA (+Audio)

MAJIBU YA TALE BAADA YA WASANII WA WCB KUTOTAJWA KWENYE FIESTA (+Audio)

| No comment
Image result for wasafi classic baby

Presha inapanda na kushuka kwa wasanii wa Bongo Fleva na Hip Hop hususan katika msimu huu wa Tamasha la Fiesta, mapigo ya moyo yanazidi kwenda mbio kwa wasanii ambao hadi sasa hawajasikika kwenye list ya wasanii watakaopanda kwenye jukwaa la Fiesta 2016.

Image result for richmavoko

Hadi sasa takriban majina 20 ya wasanii yamekwishatajwa na kusaini mkataba huku lebo kubwa ya muziki nchini inayoaminika kufanya vizuri ya WCB iliyopo chini ya Diamond Platnumz ikifanikiwa kupata shavu la msanii mmoja pekee ambaye ni Raymond atakayekinukisha katika jukwaa la Fiesta mkoani Mwanza 2016.

Kimsingi wasanii wote wa WCB kwa sasa wanafanya vizuri kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva na wote wapo kwenye ‘pick’; maswali mengi yameibuka na yanahitaji kupatiwa majibu.

Image result for raymond natafuta kiki

Katika kutaka kufahamu mapokeo ya mashabiki na watu wa karibu na lebo ya WCB, mtembezi.com imefanya mahojiano maalum na Babu Tale ambaye pia ni meneja wa ndani wa Diamond Platnumz. Tale amekubali kujibu kuhusu usahili uliofanywa kama anavyosikika kwenye sauti hapo chini.