Moro Kitaa Blog
Sorry, but you are looking for something that isn't here.
You are here:
Home
/
MUSIC NEWZ
KASSIM MGANGA AWATOLEA UVIVU MASTAA WA BONGO.
KASSIM MGANGA AWATOLEA UVIVU MASTAA WA BONGO.

Ni wazi kila msanii wa Bongo anataka kuwa mashuhuri (super star) na ndio maana kwa sasa imefika hatua walio wengi wanaishi maisha ya Instagram yaani kila kitu kinaeditiwa na kuigizwa pasipo kuwa na uhalisia.
Utakuta msanii wa muziki ama filamu anatumia muda mwingi na nguvu kubwa kuuaminisha umma na mashabiki zake kwamba ana maisha mazuri ‘classic’ wakati ukweli ni kwamba yale sio maisha yao halisi bali ni maigizo tu.
Mifano hai ipo, utakumbuka hata baadhi mastaa wa hapa nyumbani ambao tayari wamekwishatangulia mbele ya haki wakiwa na majina makubwa enzi za uhai wao walionekana kuwa na maisha ya kifahari wakati mtu hata kibanda hana, na hata kwa mastaa waliopo sasa ukweli ni kwamba maisha wanaoishi na kujionesha kupitia mitandao ya kijamii hayana uhalisia na maisha yao ya kila siku.
Hii inamfanya tajiri wa mahaba Kassim Mganga kuwatolea uvivu na kupasua jipu kwa kusema “sisi tumekuwa ‘tunafake’ vitu vingi havipo ‘real’, lakini tunataka tuwaoneshe kwenye mitandao, tunadanganya, tunawadanganya sana mashabiki wetu, mashabiki wanatuona si watu ambao tuna maisha makubwa sana, wakati haiko hivyo kiuhalisia”.