Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / JINA LA UKUTA LAZUA BALAA CHADEMA.

JINA LA UKUTA LAZUA BALAA CHADEMA.

| No comment
Image result for kamati kuu ya chadema

Oktoba 26, 2014 Vyama Vya CHADEMA, NLD, NCCR MAGEUZI na CUF vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wakiwa kwenye Viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam viongozi wa vyama hivyo walisaini rasmi mkataba wa ushirikiano uliokuwa na mambo 7 ya msingi kama nguvu pekee ya kuimarisha nguvu zao kisiasa.

Wakati vyama hivyo vikiwa ndani ya umoja huo ambao kimsingi huenda ni kama hawakufikia malengo yao basi kwali kile walichokiita“UKANDAMIZAJI WA DEMOKRASIA” CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe aliongoza Kamati Kuu ya dharura ya chama iliyoketi kuanzia Julai 23-26, 2016 Jijini Dar es Salaam na ilikuwa na ajenda moja mahsusi ambayo ni kujadili hali ya siasa na uchumi wa taifa tangu serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani mwezi Novemba 5, 2015. Ambapo kamati hiyo iliazimia na kutangaza Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA) Julai 27. Sambamba na kuitangaza Septemba 1, 2016 itakuwa siku ya maandamano na mikutano nchi nzima.

Wakati ukitafakari hilo, hoja ya msingi ni kwamba neno umoja linatokana na ushirikiano wa pamoja na kutoka pande mbili au zaidi zenye mawazo na mitazamo sawa, kwa hiyo kwa mujibu wa Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Facebook amehoji unawezaje kuuita Umoja wakati hakuna chama kingine cha upinzani kilichoshiriki mkutano na vikao vya maazimio? na kwamba neno Umoja limetimuka kimakosa.Image result for zitto kabwe

Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wameshauri kuwa badala Mbowe kutangaza kuwa kuanzia Septemba Mosi mwaka huu, itafanyika mikutano na maandamano nchi nzima basi angeweza kuitangaza kuwa ni siku ya kwenda katika kila kona ya majimbo ya CHADEMA yote na kata na mitaa walizoshinda katika Uchaguzi Mkuu uliopita kushiriki na wananchi masuala ya maendeleo ikiwemo kuendeleza na kukusanya nguvu ya pamoja katika kuboresha na kujenga miundombinu mipya ya kuchochea maendeleo, huenda kufanya kwao hivo kutawaokolea muda wa kutopambana na polisi na serikali ya Rais Magufuli na huenda kisiitwe chama cha vurugu na maandamano yasiyo na tija kama ilivyo sasa.

Hata hivyo watu wa kada mbalimbali wametoa maoni yao wakiwataka Chadema kusitisha azimio hilo la kufanya maandamano na mikutano nchi nzima kama walivyotangaza kutokana na athari zitakazojitokeza kutokana na nguvu ya polisi itakayotumika kuwazuia.JOYCE KIRIA