Followers

logo logo

SLIDE

[10] [recent] [slider-top-big] [HABARI KALI ZA WIKI]
[4] [NEWZ] [slider-top] [Habari]
You are here: Home / Jeshi la Polisi limepiga ‘STOP’ mikutano yote kisiasa nchini

Jeshi la Polisi limepiga ‘STOP’ mikutano yote kisiasa nchini

| No comment


Kutokana na matukio ya kiuhalifu yanayoendelea katika baadhi ya maeneo nchini, leo August 25 2016 Jeshi la Polisi limepiga marufuku mikutano yote ya kivyama ndani na nje ili kuzuia machafuko ya amani yanayoendelea kujitokeza katika kipindi hiki.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania,IGP Ernest Mangu amesema…>>>’Jeshi la polisi halikuzuia mikutano ya ndani ya siasa kwasababu tulikuwa tunaamini ni mikutano iliyokuwa ikizungumzia maendeleo ya wananchi
Lakini sasa tumebaini kwamba mikutano hiyo imekuwa ikitumika kucchochea wananchi na kuwahamasisha kuvunja sheria za nchi na kufanya mapambano na jeshi la polisi‘ –IGP Ernest Mangu
Kwasababu hiyo basi kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga marufuku mikutano yote ya ndani‘ –IGP Ernest Mangu